
Baada ya kuwepo kwa hatua
mbalimbali za wanafunzi wa vyuo kudai ongezeko la fedha ya kujikimu na kupatiwa
mkopo kwa wanafunzi ambao hawajapatiwa mikopo na baadae Wizara kuahidi
kushughulikia suala hilo.
Leo October 21 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli wakati ameweka jiwe la msingi katika mradi
wa ujenzi wa Hosteli za Wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam. Rais Magufuli wakati akihutubia amegusia suala la mikopo ya
wanafunzi ambapo amesema……..
‘’Vyuo
vyote vya elimu ya juu viwe na tarehe moja ya kufungua, ukishafungua kwa
haraharaka wakakaa pale kwa mwezi mmoja halafu unawaambia kufanya usajili
lazima walipe wakati bodi haijatoa orodha ya majina ya vijana watakaokopeshwa,
lazima kuwepo na mawasiliano kati ya bodi ya mikopo, TCU, wizara ya Elimu na
wizara ya fedha’’
‘’lengo la serikali si kuleta usumbufu kwa wanafunzi, lakini ni
ukweli pia haitatoa mkopo kwa wanafunzi wenye uwezo, mtoto wa Ndalichako naye
apate mkopo?, mtoto wa katibu mkuu Kijazi naye apate mkopo? haiwezekani, mkopo
huu umelenga kwa ajili ya kutoa watoto maskini lakini nasikia kule kuna
upendeleo fulani katika kutoa mkopo sasa hili Waziri na bodi zinazohusika msimamie’’alisema JPM
Comments
Post a Comment